Shabana yapokea basi jipya kutoka kwa Rais Ruto

Dismas Otuke
1 Min Read

Klabu ya Shaba FC inayoshiriki Ligi Kuu ya soka humu nchini imepokea basi jipya kutoka kwa Rais William Ruto Jumapili jioni katika hafla iliyoandaliwa katika uwanja wa Gusii.

Haya yanajiri siku moja kabla ya Rais Ruto kuanza ziara yake katika eneo la Kisii siku ya Jumatatu.

Akiwa Kisii Jumapili Ruto pia ameanzisha ujenzi wa uwanja wa michezo wa Gusii ambao umekuwa ukitumika na klabu hiyo.

Hafla hiyo ilihudhuriwa na viongozi wa kaunti za Kisii na Nyamira na pia waziri wa michezo Salim Mvurya na katibu wake Elijah Mwangi, pamoja na Katibu katika wizara ya Teknolojia ya Habari  na Mawasiliano (ICT) Stephen Isaboke.

Shabana inashikilia nafasi ya tano kwenye msimamo wa ligi kuu ya Kenya kwa alama 43 kutokana na mechi 27.

 

Share This Article