Rais William Ruto amesema serikali inaendelea kutimiza ahadi ilizotoa kwa wananchi wakati ilipochukua hatamu mwaka 2022.
Kiongozi wa taifa alisema utawala wake unajizatiti kutekeleza manifesto yake,kwa lengo kupeleka maendeleo katika sehemu zote za nchi.
“Kote nchi tunatimiza ahadi yetu kwa wananchi kwa kutekeleza manifesto na kukamilisha miradi ya maendeleo,” alisema Rais Ruto.
Aliyasema hayo alipokuwa akiweka jiwe la msingi kwa ujenzi wa soko la kisasa mjini Voi litakalogharimu shilingi milioni 300.
Kulingana na Rais, soko hilo litakuwa na vifaa vya kukabiliana na hasara ya baada ya mavuno, huku likiwahifadhi wafayabiashara 1,000.
Wakati wa ziara hiyo, Rais Ruto pia alizindua ujenzi wa uwanja wa Voi utakaogharimu shilingi milioni 950.
Uwanja huo utakuwa na uwezo wa kuwakimu watu 10,000.