kitengo cha polisi cha kudumisha usalama Nairobi kuzinduliwa mwezi Mei

kitengo hicho kitaimarisha usalama katika Jiji hilo lenye idadi kubwa ya watu, wageni na wawekezaji.

Tom Mathinji
1 Min Read
Kitengo cha polisi wa kudumisha usama Nairobi kuzinduliwa mwezi Mei.

Waziri wa Usalama wa Taifa Kipchumba Murkomen, ametangaza kuwa kitengo cha  polisi cha kudumisha usalama katika  kaunti ya Nairobi kitaanza kuhudumu Mei 1, 2026.

Murkomen aliyasema hayo leo Ijumaa, baada ya kukutana na kamati ya kiufundi inayosimamia kubuniwa na kuzinduliwa kwa kitengo hicho.

“Kuambatana na agizo la Rais William Ruto, na makubaliano ya pamoja kati ya serijkali kuu na ile ya kaunti ya Nairobi, tumejitolea kubuni kitengo cha polisi cha kudumisha usalama Nairobi kufikia Mei 1, 2026.

Kulingana na waziri huyo, kitengo hicho kitaimarisha usalama katika Jiji hilo lenye idadi kubwa ya watu, wageni na wawekezaji.

Kamati hiyo ilimuarifu waziri Murkomen kuhusu muundo unaopendekezwa, mikakati ya uongozi wake, mbinu za uzinduzi ukiwemo ufanisi muhimu ulioafikiwa.

Mkutano huo uliangazia kuimarishwa kwa ushirikiano, kuboresha utoaji huduma na kuhakikisha shughuli za kitengo hicho zinawiana na majukumu ya Huduma ya Taifa ya Polisi.

Share This Article