UDA yaandaa mchujo wake leo Ol Kalou

Dismas Otuke
1 Min Read

Kura ya mchujo kutafuta mpeperushaji bendera wa chama cha United Democratic Alliance (UDA), kwa uchaguzi mdogo wa eneo bunge la Ol Kalou, inafanyika leo Ijumaa Mei 8.

Karatasi na vifaa vya kupigia kura viliwasilishwa jana katika eneo bunge hilo tayari kwa zoezi la leo.

Wagombeaji kumi wako ulingoni kuwania tiketi hiyo moja ya UDA wakiwa;Joseph Ndirangu Ndung’u, Peter Njoroge Mugo, Samuel Muchina Nyagah, George Wambugu Kanuri (Delight) na Maina Kiambati.

Wengine wanaowinda tiketi hiyo ni; Joseph Chuchu Njuguna, Stanley Mwangi Wairimu, Mary Nyokabi Kamau, Daniel Ndung’u Mwangenye na Ezekia Kamweru Kiraing’wa.

Mshindi wa mchujo huo atapeperusha bendera ya chama tawala UDA,kwenye uchaguzi mdogo utakaoandaliwa Julai 16.

Kiti hicho kiliachwa wazi kufuatia kifo cha mbunge wa eneo hilo David Kiaraho, tarehe 29 mwezi machi mwaka huu.

Share This Article