Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Marco Rubio amesafiri Vatican siku ya Alhamisi kukutana na kiongozi wa kanisa katoliki Papa Leo wa Kumi na Nne.
Ziara hiyo ya Rubio, inajiri baada ya Rais wa Marekani Donald Trump kumkosoa vikali Papa kutokana na misimamo yake dhidi ya vita.
Kulingana na taarifa za vyombo vya habari, Rubio ambaye amejitambulisha kuwa Mkatoliki mwenye imani thabiti, alijaribu kupunguza tofauti zilizopo kati ya Trump na Vatican kabla ya mkutano huo wa faragha.
Katika kuendeleza ziara yake, Rubio alikutana na kuzungumza na Kardinali Pietro Parolin, Katibu wa Jimbo la Vatican.
Balozi wa Marekani katika Vatican alikuwa amesema awali kuwa mkutano huo ungetarajiwa kuwa na mazungumzo ya wazi na ya moja kwa moja.
Kardinali Pietro Parolin aliwaambia waandishi wa habari Vatican jana kuwa watasikiliza kile ambacho mgeni wao atakisema, akibainisha kuwa mkutano huo umefanyika kwa ombi la Washington.
Taarifa ya BBC