Offset aendelea kupata nafuu baada ya kupigwa risasi

Msemaji wake aliambia wanahabari kwamba majeraha yake sio ya kutishia maisha.

Marion Bosire
1 Min Read

Mwanamuziki wa mtindo wa Rap nchini Marekani Kiari Kendrell Cephus, maarufu kama Offset anaendelea kupata nafuu hospitalini saa kadhaa baada yake kupigwa risasi kwa mujibu wa msemaji wake.

Offset wa umri wa miaka 34 alipigwa risasi nje ya Casino moja huko Florida nchini Marekani Jumatatu usiku dakika chache baada ya saa moja, kulingana na saa za Marekani.

Polisi wa Seminole walithibitisha kisa hicho wakisema kwamba walikamata washukiwa wawili kuhusiana nacho na uchunguzi unaendelea.

Offset anafahamika kwa kuwa mmoja wa wanachama wa kundi la watatu la muziki, mtindo wa Hip-Hop la Migos wengine wakiwa Quavo na Takeoff. Kundi hilo lilisambaratika mwanzo wa mwaka 2022.

Quavo na Takeoff baadaye waliamua kuwa kundi la wawili lenye jina Unc & Phew huku Takeoff akiamua kuimba peke yake.

Takeoff alipigwa risasi na kuuawa mwezi Novemba mwaka 2022.

Share This Article