Watu wawili wafariki kwenye maandamano Siaya

Tom Mathinji
1 Min Read
Watu wawili wafariki kwenye maandamano Siaya..

Watu wawili waliuawa siku ya Jumatatu  katika eneo la Gem–Ramula, kaunti ya Siaya, kufuatia maandmano ya ghasia kupinga mipango ya kufurushwa kwa wakazi kulikohusishwa na kampuni ya Shanta Gold Kenya Limited.

Duru zinaarifu kuwa  wawili hao walikuwa sehemu ya kundi kutoka kaunti jirani ya Vihiga ambao walikuwa wakiandamana kupinga uwepo wa kampuni hiyo ya uchimbaji dhahabu.

Wakazi waliandamana wakitaka kubatilishwa kwa mpango huo, lakini taharuki ilizidi na kusababisha vifo hivyo. Maafisa wa utawala katika sehemu hiyo hata hivyo hawakutoa maelezo kuhusu kiini cha vifo hivyo.

Tukio hilo limeibua upya wasiwasi kuhusu mizozanao ya kijamii na mizozo ya ardhi katika sehemu hiyo. Aidha maafisa wa usalama walifanikiwa kuzima jaribio la waandamanaji kuvamia kituo cha polisi cha  Ramula.

Kipande cha ardhi cha ekari 1154 kinachozozaniwa kwa upande mmoja kipo katika kaunti ya Siaya na upande wa pili katika kaunti ya Vihiga kwenye soko la Ramula.

Share This Article