Kapteni wa zamani wa Harambee Stars Victor Wanyama, astaafu kutoka soka

Dismas Otuke
1 Min Read

Kiungo mkabaji na aliyekuwa nahodha wa timu ya taifa Kenya,Harambee Stars Victor Wanyama,amestaafu  soka  ya kulipwa baada ya kuvalia daluga  kwa takriban miaka 19.

Wanyama alitangaza kustaafu kwake rasmi siku ya Ijumaa kupitia mitandao yake ya kijamii, akiwashukuru wote waliomuunga mkono katika amali yake .

Wanyama alichezea vilabu vya City  Stars , AFC Leopards na Helsinborg ya Uswidi baina ya 2006 na 2008, akiwa chipukizi.

Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 34, alianza kupiga soka ya kulipwa mwaka 2008, na klabu ya Beerschot ya Ubelgiji na baadaye Celtic  ya Scotland hadi  mwaka 2013.

Mwaka-2013-2016 Wanyama alijiunga na Southampton akiwa Mkenya wa kwanza kucheza ligi kuu Uingereza.

Baadaye aliwasili Tottenham Hotspur alikosakata soka kwa miaka minne kutoka 2016 hadi  2020,kabla ya kujinga na CF Montreal ya Canada kwa miaka minne 2020 hadi 2024.

Alirejea Sctotland mwaka 2025 akiicheze klabu ya divisheni ya pili ya Dumfernmille .

Katika timtaifa,taifa Wanyama alipiga mechi 64 baina ya mwaka 2007 na 2020, akipachika magoli 6.

Kwa jumla,kwenye amali yake Wanyama alititiga michuano 387, katika kiwango cha klabu na kufunga mabao 27.

Share This Article