Duale afungua kongamano la kimataifa la afya ya kina mama na watoto

Waziri alikariri kujitolea kwa serikali kuhakikisha upatikanaji wa huduma bora za afya kwa wote, wakiwemo kina mama na watoto.

Dismas Otuke
1 Min Read

Waziri wa Afya Aden Duale amefungua kongamano la kimataifa kuhusu afya ya kina mama na wtoto  (IMNHC) jijini Nairobi.

Duale aliyemwalikilisha Rais William Ruto, alikariri kujitolea kwa serikali kuhakikisha upatikanaji wa huduma bora za afya kwa wote, wakiwemo kina mama na watoto.

Alitaja baadhi ya ufanisi wa serikali katika afya ikiwemo kurahisisha utoaji wa huduma za  afya kwa  wajawazito na watoto, na utoaji chanjo kwa watoto.

Waziri alitaja hatua ziizopigwa na serikali ya Rais Ruto tangu kuanzishwa kwa bima mpya ya matibabu ya SHA, ambayo tayari imewasajili Wakenya zaidi ya milioni 30 kufikia sasa.

Kongamano hilo liliwaleta pamoja Mawaziri wa Afya kutoka barani afrika akiwemo Douglas Tendai Mombeshora wa Zimbabwe na Dkt. Dereje Duguma wa Ethiopia.

Katibu wa Afya ya Umma nchini Mary Muthoni na Mkurugenzi wa Afya Dkt. Patrick Amoth ni miongoni mwa waliohudhuria.

Share This Article