Matumaini ya timu ya Kenya ya wanaume ya raga kwa wachezaji saba upande kutwaa taji la kwanza la mashindano ya msururu wa dunia divisheni ya pili, yalididimia baada ya kuambulia kichapo cha alama 12-7 kutoka kwa Ujerumani Jumapili usiku mjini Montevideo nchini Uruguay.
Kenya watafunga ratiba ya mashindano hayo kwa mechi dhidi ya wenyej Uruguay mapema Jumatatu.
Shujaa tayari wamepoteza mechi mbili kufikia sasa baada ya kushindwa na Marekani katika mechi ya ufunguzi siku ya Jumamosi.