Monica Kathina Juma, ambaye ni Mshauri wa Taifa wa maswala ya Usalama, ameteuliwa kwenye nyadhifa mbili Kuu katika Umoja wa Mataifa.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres, alimteua Juma kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa afisi ya Umoja wa Mataifa kuhusu Mihadarati na Uhalifu (UNODC) na Mkurugenzi Mkuu katika afisi ya Umoja wa Mataifa ya Vienna (UNOV).
Anachukua wadhifa ulioshikiliwa na Ghada Fathi Waly.
Juma ambaye ni kiongozi tajika, ana tajiriba ya muda mrefu katika utungaji wa sera za umma, utekelezaji na msomi katika maswala ya Usalama, diplomasia na uongozi.
Awali Juma amehudumu wadhifa wa Waziri katika wizara za Nishati (2021-2022); Wizara ya Ulinzi (2020-2021); Wizara ya Mambo ya Nje (2018-2020), kaimu Waziri wa petroleum na madini (2022).
Vile vile aliwahi hudumu kama Katibu katika wizara ya Mambo ya Nje (2016-2018), Wizara ya Usalama wa Taifa (2014-2016), na wizara ya Ulinzi (2013-2014).