Shughuli ya ujumuishaji na uhesabu wa kura imeanza katika uchaguzi mdogo wa eneo bunge la Ol Kalou.
Vituo vya kupigia kura vilifungwa Alhamisi saa kumi na moja jioni huku idadi ndogo ya ya wapigaji kura chini ya asilimia 60 ikijitokeza.
Mwaniaji wa upinzani wa chama cha DCP Sammy Ngotho, anaongoza katika vituo vingi vya ujumuishaji kura .
Vituo kvingi vya kupigia kura vilishuhudia utulivu, huku vichache vikikumbwa na vurumai na ghasia.
Kiti hicho kiliachwa wazi kufuatia kifo cha aliyekuwa Mbunge David Njuguna Kiaraho,Machi 29, mwaka huu akiwa na umri wa miaka 62,akipokea matibabu katika ikulu ya Nairobi.