Shirikisho la kandanda barani Afrika -CAF limeongeza zawadi ya pesa kwa mashindano baina ya vilabu kuanzia msimu huu ambao unaelekea hatua ya robo fainali.
Washindi wa kombe la Ligi ya Mabingwa watatuzwa shilingi milioni 768 kutoka shilingi milioni 512 za awali.
Hata hivyo, zawadi ya pesa kwa timu itakayomaliza ya pili itasalia shilingi milioni 256, huku watakaoshindwa katika nusu fainali wakibugia shilingi 153.6 kila mmoja.
Timu zitakazobanduliwa katika robo fainali zitapokea shilingi milioni 115.2, ilihali watakaomaliza katika nafasi za tatu na nne kwenye makundi wakituzwa shilingi milioni 89. 6.
Mabingwa wa kombe la shirikisho watazawadiwa shilingi milioni 512 ,wakati watakaomaliza nafasi ya pili wakitia kibindoni shilingi milioni 128.
Timu zitakazoaga mashindano katika nusu fainali zitapokea shilingi milioni 96 na shilingi milioni 70.4, kwa watakaoshindwa katika robo fainali.
Vilabu vitakavyochukua nafasi za tatu na nne katika hatua ya makundi vitazawadiwa shilingi milioni 51.2 kila moja.