Waziri wa fedha Njuguna Ndung’u amemteua Humphrey Wattanga Mulongo kuwa kamishna mkuu wa mamlaka ya kukusanya ushuru nchini KRA.
Kwenye arifa ya gazeti rasmi la serikali hivi leo, waziri Ndung’u alielezea kwamba Mulongo atahudumu kwenye wadhifa huo kwa muda wa miaka mitatu.
Bodi ya mamlaka ya kukusanya ushuru nchini KRA ilitangaza kujiuzulu kwa aliyekuwa kamishna mkuu wa KRA Githii Mburu, Februari mwaka huu.
Rispar Simiyu aliteuliwa kaimu kamishna mkuu wa KRA baada ya kujiuzulu kwa Githii.
Mulongo alisomea biokemia katika chuo kikuu cha Harvard huko Marekani na baadaye akaingia chuo cha Wharton ambapo alifuzu na shahada ya uzamili katika usimamizi wa biashara.
Awali alifanya kazi nchini Marekani na Afrika Kusini kabla ya kurejea nchini Kenya takribani miaka 10 iliyopita.