Mwakilishi Wanawake wa Kirinyaga ajeruhiwa kwenye vurugu Kerugoya

Martin Mwanje & Leonard Munene
1 Min Read
Makabiliano makali yalishuhudiwa katika mji wa Kerugoya, kaunti ya Kirinyaga baada ya uhasama kuzuka kati ya makundi mawili pinzani ya kisiasa.
Tandabelua hiyo inasemekana kumwacha mwakilishi wa wanawake katika kaunti hiyo Jane Njeri akiuguza majeraha kiasi kwamba alikimbizwa hadi hospitalii ya rufaa ya Kerugoya ili kupewa matibabu.
Kizaazaa kilianza pale Njeri akiandamana na mwakilishi wadi wa Baragwi David Mathenge na wafuasi wao waliandamana kuelekea ofisi za Idara ya Upelelezi wa Jinai, DCI tawi la Kerugoya kulaani madai dhidi ya Mathenge.
Mathenge anatuhumiwa kwa kufungua kisima cha Mukandu katika wadi ya Kanyekini kinyume cha sheria.
Vurugu zilianza wakati kundi linaloaminika kuwa la kambi pinzani lilipojitokeza na kukabiliana na lile la Mathenge.
Hata hivyo, baada ya kisa hicho, wafuasi wa Gavana wa kaunti ya Kirinyaga Anne Waiguru walilaani viongozi ambao wamekuwa mwiba kwa utawala wa kaunti hiyo kwa kupinga mapendekezo ya miradi ya maendeleo.
Martin Mwanje & Leonard Munene
+ posts
Share This Article