Mwakilishi wa Wanawake wa zamani wa Kajiado afariki

Martin Mwanje
1 Min Read
Janet Marania Teyiaa - Mwakilishi wa Wanawake wa zamani wa Kajiado

Mwakilishi wa Wanawake wa zamani wa kaunti ya Kajiado Janet Marania Teyiaa amefariki.

Rais William Ruto amemwomboleza Teyiaa akimtaja kuwa kiongozi aliyekuwa maarufu kwa kipindi alichohudumu kwenye wadhifa huo.

“Teyiaa alikuwa mtumishi wa umma aliyekuwa na shauku na kiongozi mashuhuri aliyetumikia watu wake kwa kujitolea,” alisema Rais Ruto kwenye risala yake ya rambirambi.

“Alikuwa mwanatimu asiyekuwa mbinafsi na mtu wa kuigwa aliyewatia wengi moyo wa kutimiza ndoto zao licha ya kutoka kwa familia isiyojiweza.”

Kiongozi wa nchi ameifariji familia ya marehemu, marafiki na watu wa Kajiado kutokana na kifo cha mwendazake aliyemtaja kama kiongozi shupavu.

 

Website |  + posts
Share This Article