Mr. Blue aadhimisha miaka 22 kama mwanamuziki

Mr. Blue alisema kwamba anatoa nyimbo 22 kwa ajili ya kusherehekea muda wake katika muziki.

Marion Bosire
1 Min Read

Khery Sameer Rajab ambaye ni msanii wa muziki nchini Tanzania ambaye wengi wanamfahamu kama Mr. Blue anaadhimisha miaka 22 katika tasnia ya muziki.

Akizungmza na wanahabari kwa mara ya kwanza kabisa maishani mwake katika hoteli ya Hekima Garden huko Mikocheni, Dar es Salaam jana, Mr. Blue alisema kwamba anatoa nyimbo 22 kwa ajili ya kusherehekea muda wake katika muziki.

Msanii huyo alisema pia kwamba nyimbo hizo ni njia ya kushukuru mashabiki wake ambao wamemuunga mkono kwa muda mrefu.

Kuhusu kutoandaa vikao na wanahabari mara kwa mara kama wasanii wengine, Mr. Blue alielezea kwamba yeye hapendi mahojiano na wanahabari kutokana na maisha aliyowahi kupitia katika safari yake ya muziki.

Mkali huyo wa Bongo Fleva alitangaza pia uzinduzi rasmi wa studio yake kwa jina “Blue Records” ambayo alisema itasaidia wasanii wengine hasa wanaoibuka.

Alifichua kwamba nyingi kati ya nyimbo zake 22 zimerekodiwa kwenye studio hiyo, akisema atakuwa anazitoa kwa awamu ambapo jana pekee aliahidi kutoa video nne.

Lakini kufikia sasa, nyimbo alizochapisha kwenye akaunti yake ya YouTube kufikia sasa ni tatu na ni ‘Rasta’, ‘Tutoke’ na ‘Mr. Maujuzi’ ambao amemhusisha msanii Barnaba.

Website |  + posts
Share This Article