Watu saba wa familia moja waangamia kwenye ajali Mai Mahiu

Waliofariki ni pamoja na watoto wanne na watu wazima watatu.

Dismas Otuke
0 Min Read

Watu saba wa familia moja waliangamia kwenye ajali ya barabarani katika barabara kuu ya Naivasha-Mai Mahiu jana usiku.

Kulingana na polisi, saba hao walikuwa wakirejea kutoka kwa ukumbusho wakati gari lao lilipogongana na lori kutoka nyuma na kufariki papo hapo.

Waliofariki ni pamoja na watoto wanne na watu wazima watatu.

Polisi wamesema wameanzisha uchunguzi kubaini chanzo cha ajali hiyo.

Website |  + posts
Share This Article