Wanamuziki wa kimataifa wa Reggae kuandaa tamasha la kusaidia wasioweza kusikia

Mapato yatakayotokana na tamasha hilo yatatumiwa kupiga jeki mipango muhimu ya jamii za walemavu wa kusikia zilizotelekezwa katika kaunti ya Kwale na Nairobi.

Marion Bosire
1 Min Read

Wanamuziki wa mtindo wa reggae wanaogahamika kimataifa Alborosie na Don Campbell watakuwa watumbuizaji wakuu katika tamasha litakaloandaliwa Februari 15, 2025 la kusaidia walemavu wa kusikia nchini.

Tamasha hilo litaandaliwa katika ukumbi wa Tsavo katika jumba la KICC jijini Nairobi na litahusisha wasanii wa humu nchini Nazizi, Kevin Wyre na bendi ya Gravitti.

Waandalizi wa tamasha hilo ni The Long Trail, kituo cha walemavu wa kusikia cha Kwale, Mtaani.com na King Lion Sounds na wanalenga kukabiliana na dhana potovu za walemavu wa kusikia na kuonyesha uwezo wao.

Watakaohudhuria watakuwa na fursa ya kutagusana na walemavu wa kusikia kupitia vikao vya mafunzo ya lugha ya ishara, kupata huduma za kuagiza chakula kutoka kwa walemavu hao na vituo vya kuhusiana nao kwa lengo la kuhimiza ujumuishaji.

Meneja wa The Long Trail Jos Wesemann anahisi kwamba kwa kuwa inaongozwa na Don Campbell na Alborosie hafla hiyo inaonyesha sio tu muziki lakini pia ushirikiano wa kuleta mabadiliko.

Mapato yatakayotokana na tamasha hilo yatatumiwa kupiga jeki mipango muhimu ya jamii za walemavu wa kusikia zilizotelekezwa katika kaunti ya Kwale na Nairobi.

Tiketi za shughuli hiyo ya februari 15, 2025 sasa zinapatikana kwenye tovuti ya Mtaani.com na habari zaidi zinapatikana kwenye tovuti www.thelongtrail.travel.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *