Dkt. Ronoh: Sekta ya mboga na matunda ni muhimu kwa ukuaji wa uchumi

Dr. Yusuf Muchelule
1 Min Read
Katibu katika wizara ya kilimo Dr. Kipronoh Ronoh.

Katibu katika Wizara ya Kilimo Dkt. Kipronoh Ronoh amesema kuwa ufufuzi wa sekta ya mboga na matunda utafanikisha uthabiti wa uchumi wa taifa hili.

Kulingana na katibu huyo, kupitia ufufuzi wa sekta hiyo, serikali itahakikisha maslahi ya wadau wote yanashughulikiwa ipasavyo ili kuboresha zaidi ukuaji wake.

Dkt. Ronoh aliyasema hayo Jumanne, alipozindua rasmi kamati ya kitaifa kuhusu mboga na matunda itakayoongozwa na Dkt. Collins Marangu kutoka Wizara ya Kilimo, huku naibu wake akitoka katika sekta ya kibinafsi.

Kamati ya kitaifa iliyobuniwa kustawisha sekta ya mboga na matunda

Kamati hiyo inatarajiwa kushughulikia kikamilifu changamoto zinazoghubika sekta ya mboga na matunda pamoja na ile ya maua hapa nchini.

“Kamati hiyo ya kitaifa inapaswa kutoa mwongozo kuhusu jinsi ya kukabiliana na changamto ibuka katika sekta hiyo,” alisema Dkt. Ronoh.

Aliongeza kuwa atashirikiana na kamati hiyo pamoja na asasi zingine za serikali kukabiliana na changamoto hizo.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *