Rais William Ruto amekutana na Magavana kutoka kaunti za eneo la Mlima Kenya katika Ikulu ya Nairobi, kuzungumzia maendeleo jumuishi.
Mazungumzo ya Rais na viongozi hao pamoja na viongozi wengine wakuu serikalini yalijikita katika kuangazia mahitaji ya wananchi, maendeleo na kuhimiza ukuaji wa kimaendeleo kwa maeneo yote nchini.
Kikao hicho kilihudhuria na Naibu Rais Kithure Kindiki, Magavana Cecily Mbarire, kutoka Embu, Anne Waiguru wa Kirinyaga, Kimani Wamatangi wa Kiambu, Joshua Irungu wa Laikipia, Muthomi Njuki wa Tharaka Nithi, Irungu Kang’ata wa Murang’a, Kiarie Badilisha wa Nyandarua na Isaac Mutuma kutoka Meru.
Kikao hicho kinajiri chini ya wiki moja baada ya Rais pia kukutana na viongozi waliochaguliwa kutoka eneo la mlima Kenya kwenye ikulu ya Nairobi.