Azma ya timu ya taifa ya Kenya, Harambee Stars, kufuzu kwa fainali ya makala ya mwaka huu ya Kombe la Mapinduzi iliyeyuka baada ya kuzabwa bao moja kwa bila na wenyeji Zanzibar jaa usiku katika uwanja wa Gombani.
Bao pekee na ushindi kwa wenyeji lilitiwa kimiani na Ali Khatib kunako dakika 94, huku jumla ya kadi tisa za njano na mbili nyekundu zikitolewa.
Nahodha wa Kenya Aboud Omar alipigwa kadi nyekundu baada ya kuteta kuhusu maamuzi ya refa.
Zanzibar waliomaliza wa pili kwa alama 6, moja nyuma ya Burkina Faso, sasa watarejea uwanjani Januari 13 dhidi ya Burkina Faso kwenye fainali.
Kenya ilimaza ya tatu kwa pointi nne baada ya kutoka sare ya bao 1 dhidi ya Burkina Faso na kuizaba Tanzania 2-0.