Kinara wa chama cha Wiper Kalonzo Musyoka amesisitiza kuwa viongozi wote wanaogemea mrengo wa Naibu Rais wa zamani Rigathi Gachagua wataungana ili kuhakikisha wanambandua Rais William Ruto madarakani.
Akizungumza akiwa mjini Nanyuki leo Jumatatu, Kalonzo alidai nchi hii imefilisika kutokana na wizi wa fedha za mma unaofanywa na utawala wa sasa na kamwe hatakaa kitako na kutazama uovu huo ukiendelea.
Kulingana naye, masuala ya utekaji nyara ni jambo lingine linalopaswa kushunghulikiwa na akiongeza kwamba kuungana kwao kuungana kwao viongozi wengine kutahakikisha umoja wa nchi.
Kalonzo anaituhumu serikali ya sasa kwa kuyatenga maeneo mengine katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
Wakati wa ziara yake mjini Nanyuki, ofisi za chama cha Wiper zilifunguliwa kwa mara ya kwanza mjini humo wakati akimezea mate uungwaji mkono wa eneo la Mlima Kenya katika azma yake ya kuwania urais.