Mamia waandamana Korea Kusini kumuunga mkono Yoon anayekabiliwa na tishio la kukamatwa

Martin Mwanje
1 Min Read

Mamia ya wafuasi wa Rais alieyondolewa madarakani wa Korea Kusini Yoon Suk Yeol waliandamana nje ya makazi yake leo Jumatano huku wapelelezi wakianzisha juhudi mpya za kumkamata. 

Yoon amekataa kuhojiwa na kukamatwa tangu hatua yake iliyotibuka ya kutangaza sheria ya kijeshi Disemba 3 kuitumbukiza Korea Kusini katika janga baya la kisiasa katika kipindi cha miongo kadhaa iliyopita.

Wapelelezi walipata kibali kipya cha kukamatwa kwake baada ya muda wa agizo la awai la siku saba kukamilika.

Mamia ya watu walielekea kwenye makazi ya rais katikati mwa mji wa Seoul wakistahimili kijibaridi kikali.

“Idadi kubwa ya watu wanakuja kujiunga nasi. Licha ya baridi kali, wengi walikesha usiku kucha,” alisema Lee Hye-sook, mfuasi wa Yoon mwenye umri wa miaka 57 wakati akizungumza na AFP nje ya makazi ya rais.

Kwa upande mwingine, waandamanaji wanaotaka Yoon aadhibiwe walipunga vijiti vilivyong’aa  — ambavyo kwa kawaida huonekana kwenye matamasha ya  K-Pop — na kubeba mabango yaliyokuwa na maandishi yaliyosema, “Mkamate muasi Yoon Suk Yeol”.

Timu ya wanasheria wa Yoon ilisema leo Jumatano kuwa anasalia kwenye makazi yake baada ya wapelelezi siku iliyotangulia kutilia shaka aliko.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *