Mahakama yawapa wanafunzi afueni Kakamega

Kbc Digital
1 Min Read

Ni afueni kwa wanafunzi 1,200 kutoka familia maskini katika Kaunti ya Kakamega baada ya mahakama kuagiza kanisa la Friends Church Amalemba kufungua afisi za shirika lisilokuwa la kiserikali la United Kenya Rising ambalo limekuwa likifadhili masomo yao.

Kanisa hilo lilikuwa limefunga afisi za shirika hilo baada ya mzozo kuibuka baina yao.

Mahakama ya Kakamega kupitia kwa Hakimu Mkuu Mkazi Vienah Amboko imesikiza kesi hiyo na kuamuru afisi hizo zilizopo kwenye kanisa hilo, zifunguliwe kwa siku tatu ili wanafunzi husika waweze kulipiwa karo.

Wakili wa shirika hilo, Wellington Adeki, na Mkurugenzi wake, Nelson Idah, wameridhika na uamuzi wa mahakama.

Kesi hiyo itatajwa tena mnamo tarehe 26 Februari mwaka huu.

Taarifa ya Carolyn Necheza 

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *