Kaunti ya Kisumu itaandaa makala ya kwanza ya mashindano ya soka baina ya shule nane bora za sekondari kwa wavulana nchini maarufu kama Super 8 kati ya Februari 1 na 2.
Mashindano hayo yatashirikisha shule zilizo na mataji mengi katika mashindano ya kitaifa na limbukeni katika mchezo wa soka.
Kundi A, linajumuisha mabingwa mara 12 wa taji ya Kitaifa kutoka magharibi Kakamega school ( Green commandoes),mabingwa wa kitaifa mwaka jana Highway kutoka Nairobi, Ringa ya Nyanza na Ongata Academy ya Bonde la Ufa.
Kundi B lina mabingwa wa kitaifa mara sit St. Antony Boys ya Bonde la Ufa, Kisumu Day kutoka Nyanza, Ambira ya Nyanza na Bukembe kutoka Magharibi.
Dimba hili litasakatwa katika nyuga za Mamboleo na Moi washiriki wakiyatumia mashindano kujinoa makali kwa kindumbwendumbwe baina ya shule za upili baadaye mwaka huu.
Taarifa ya Boniface Musotsi