Odede kuzikwa Januari 18 kaunti ya Siaya

Dismas Otuke
1 Min Read
Roseline Odede - Marehemu Mwenyekiti wa KNCHR

Aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Kitaifa ya Haki za Kibinadamu (KNCHR) Roseline Odede atazikwa Januari 18 kijijini Ruma, kaunti ya Siaya.

Familia ya marehemu hata hivyo imesema itatoa taarifa zaidi za mipango ya mazishi baadaye.

Odede alifariki Januari 3 mwaka huu  baada ya kuugua kwa muda mfupi.

Marehemu alikuwa mkewe Dkt. Joram Odede na amewaacha watoto wawili, Clara Odede na Diane Odede.

Hadi kifo cahke, Odede alikuwa wakili wa Mahakama Kuu ya Kenya na mpatanishi.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *