Mwanamume ahukumiwa miaka 4 gerezani kwa kumiliki risasi kinyume cha sheria

Wako Ali
1 Min Read
Mwanamume ahukumiwa miaka 4 gerezani kwa kumiliki risasi kinyume cha sheria.

Mahakama ya Marsabit imempata mwanamume mmoja na makosa ya kumiliki risasi kinyume cha sheria na kumhukumu kifungo cha miaka 4 gerezani.

Mohamed Mutua Hassan alipatikana na makossa ya kumiliki risasi nne,bila kuwa na kibali cha kumiliki silaha hizo.

Hukumu hiyo imetolewa na Hakimu Mkuu wa Mahakama ya Marsabit Bi Christine Wekesa.

Hata hivyo mstakiwa ana siku 14 za kukata rufaa.

Upande wa mashtaka uliambia mahakama kuwa mnamo  Mei 5, 2023,  Mohamed Mutua Hassan alipatikana na silaha hizo nyumbani kwao katika mtaa wa Wabera, mjini Marsabit.

Akijitetea mshtakiwa alikana mashtaka akisema kuwa sihaha hizo hazikupatikana nyumbani kwake ila kwa babake ambaye sasa ni marehemu.

Hata hivyo mahakama ilipuuzilia mbali madai hayo.

Vile vile mshtakiwa alitaka mahakama kumsameha akisema ana watoto wachanga ambao wanamtegemea.

TAGGED:
Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *