Ndege ya abiria yaanguka Kazakhstan na kuua watu wanne

Ndege hiyo ilikuwa safarini kutoka Azerbaijan kulekea Russia ilipoanguka karibu na mji wa Aktau nchini Kazakhstan.

Marion Bosire
1 Min Read

Ndege ya abiria iliyokuwa safarini kutoka Azerbaijan kulekea Russia ilianguka karibu na mji wa Aktau nchini Kazakhstan, na kuua watu wanne kulingana na taarifa za wahudumu wa afya.

Ndege hiyo nambari ilikuwa na abiria 62 na wahudumu watano na ililazimika kutua ghafla kilomita tatu kutoka Aktau.

Watu 29 wakiwemo watoto wawili waliponea ajali hiyo na kupelekwa hospitalini kulingana na taarifa ya wizara ya dharura ya Kazakhstan.

Awali wizara hiyo ilikuwa imetangaza manusura kuwa 25, lakini baadaye ikabadili idadi hiyo kuwa 27, 28 na mwisho watu 29, wakati shughuli za uokoaji zilikuwa zikiendelea.

Shirika la habari la Urusi la Interfax liliripoti kwamba miili minne ilitolewa katika eneo la tukio.

Wizara ya dharura ilisema kwamba moto uliowaka kwenye ndege hiyo ilipokuwa ikitua ulizimwa na wahudumu wa zima moto wapatao 150.

Waendeshaji wa ndege hiyo wanaripotiwa kuomba kutua katika eneo tofauti kabla ya ajali kutokea kutokana na kile walichokitaja kuwa ukungu mwingi huko Grozny.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *