Wakimbizi kambi ya Kakuma waandamana, walalamikia uhaba wa chakula

KBC Digital
1 Min Read
Wakimbizi waandamana katika kambi ya Kakuma, walalamikia uhaba wa chakula na maji

Maelfu ya wakimbizi katika kambi ya Kakuma walifanya maandamano wakitoa wito wa kuchukuliwa kwa hatua za haraka kuhusiana na uhaba mkubwa wa chakula na maji unaoshuhudiwa kambini hapo.

Maandamano hayo yalifuatia upunguzaji wa hivi karibuni wa msaada wa kibinadamau, ambao kwa kiwango kikubwa ulisababishwa na kupunguzwa kwa  ufadhili wa Shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa (USAID).

Shirika hilo ni mfadhili mkubwa wa mipango ya wakimbizi nchini Kenya.

Kulingana na wakazi, hali katika kambi hiyo zimezorota huku wengi wakihangaika kupata bidhaa muhimu.

“Hatujala kwa siku kadhaa, na sasa maji pia imekuwa bidhaa adimu. Watu wanateseka, na inaonekana hakuna anayesikiliza,” alilalama Rita Namrembe.

Shirika la Umoja wa Mataifa la Wakimbizi (UNHCR) na Mpango wa Chakula Duniani (WFP), yanayosimamia usambazaji wa bidhaa za msaada katika kambi ya Kakuma, awali yalionya kuwa uhaba wa fedha unaweza ukayalazimu kupunguza shughuli zao.

Katika miezi ya hivi karibuni, mgao wa chakula umepunguzwa kwa kiasi kikubwa na kufanya maisha kuwa magumu zaidi katika kambi ya Kakuma.

KBC Digital
Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *