Angola, Madagascar, Sudan, Cote d’Ivoire na Sudan zanusia tiketi za CHAN mwakani

Dismas Otuke
1 Min Read

Mataifa ya Angola, Angola, Madagascar, Sudan, Cote d’Ivoire na Sudan yalijiweka katika nafasi nzuri ya kufuzu kwa makala ya nane ya fainali  za Afrika kwa wachezaji wa nyumbani.

Katika matokeo ya mechi za Jumamosi na Jumapili za mkumbo wa kwanza wa raundi ya tatu, Cote d’Ivoire iliwazabua Burkina Faso 2-0 katika uchanjaa wa Félix Houphouët-Boigny, Sudan ikaititiga Ethiopia magoli 2-0 huku Mauritania ikiwalemea Mali bao 1-0 .

Cameroon waliisakama Jamhuri ya Afrika ya Kati bao moja bila jawabu.

Sudan Kusini iliwamenya Rwanda 3-2, Ghana na Nigeria wakaambulia sare huku mabingwa watetezi Senegal wakitoka sare ya 1-1 dhidi ya Liberia.

Angola wakicheza ugenini walilaza Lesotho 2-0, Zambia ikaikomoa Msumbiji magoli 3-0 huku Madagascar pia ikiwaadhibu Eswatini 3-0 ugenini.

Equatorial Guinea na Congo zilitoka sare kappa kisha Niger na Togo watoka sare ya 1-1.

Mechi za marudio zitachezwa kuanzia Disemba 25 huku washindi wa jumla wakifuzu kwa fainali za AFCON zitakazoandaliwa Kenya, Uganda na Tanzania kati ya Februari mosi na 28 mwakani.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *