Mlipuko wa kipindupindu waripotiwa Migori, watu 8 walazwa

Martin Mwanje
1 Min Read

Watu wanane wamebainika kuambukizwa ugonjwa wa kipindupindu katika kaunti ya Migori.

Afisa mkuu wa kaunti hiyo anayesimamia afya ya umma Mabele Chanzu amesema wanane hao walilazwa katika hospitali ya rufaa wakiwa katika hali mahututi lakini kwa sasa hali yao imeimarika.

Chanzu amesema wameongeza uangalizi wa afya katika kaunti hiyo ili kudhibiti mlipuko wa ugonjwa huo.

Kauli sawia zimetolewa na mwenzake katika idara ya elimu Betty Samburu ambaye ametoa wito kwa wasimamizi wa shule kutahadhari hasa kwa vyakula vinavyouzwa karibu na ua.

Mlipuko huo unakuja wakati raia wa kaunti hiyo wakihangaika kupata maji safi na huduma zingine muhimu.

Tangu kuanza kwa mlipuko huo mnamo mwezi Oktoba mwaka jana, Wizara ya Afya na washirika wake ikiwa ni pamoja na Shirika la Msalaba Mwekundu ilitia juhudi za kudhibiti na kuzuia kusambaa kwa ugonjwa huo katika kaunti hiyo.

Visa vya kuenea kwa ugonjwa wa kipindupindu kwa kasi viliripotiwa kufuatia sherehe za msimu wa Krismasi na pirikapirika za watu kusafiri katika kaunti 25 zilizokuwa zikiripoti visa kufikia mwaka huu.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *