Shujaa taabani baada ya kupoteza mechi mbili Vancouver

Dismas Otuke
1 Min Read

Timu ya taifa ya raga ya Kenya kwa wachezaji saba kila upande maarufu kama Shujaa, imejipata kwenye njia panda baada ya kushindwa mechi mbili za kundi A katika mkondo wa nne wa Vancouver mapema Jumamosi.

Kenya ilifungua mashindano kwa kipigo cha alama 24-0 kutoka kwa Argentina, kabla ya kulemewa na Ufaransa alama 33-7 katika mchuano wa pili.

Shujaa watarejea uwanjani kwa mechi ya mwisho ya makundi dhidi ya Uiengereza leo usiku kabla ya kucheza mechi za uorodheshaji.

Kenya inakabiliwa na hatari ya kushushwa daraja ikiwa ya 9 kwenye msimamo wa dunia baada ya misururu mitatu kwa alama 14.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *