Kenya Airways yazindua ndege mpya kupiga jeki huduma

Dismas Otuke
0 Min Read

Kampuni ya ndege nchini Kenya Airways (KQ) imezindua ndege mpya aina ya Boeing 737-800 kuboresha utoaji huduma.

Ndege hiyo inayobeba abiria 170 imekodiwa kutoka kampuni ya Dubai Aerospace Enterprise na kufikisha jumla ya ndege 35 zinazomilikiwa na KQ.

Afisa mkuu mtendaji wa KQ Allan Kilavuka, amesema wanalenga kukuza biashara yao ili kushinda vyema na wapinzani.

Aidha Kilavuka amesema wameanza mikakati ya kupanua biashara za usafirishaji mizigo.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *