Jumla ya Wakenya 1,848 walituma maombi ya Uenyekiti wa tume huru ya uchaguzi na uratibu wa mipaka nchini (IEBC)./strong>
Jopo la uteuzi limesema watu hao walituma maombi ya kazi hiyo kupitia kwa barua pepe na ni pia barua.
Mwenyekiti wa Jopo la Uteuzi Nelson Makanda, amesema tayari wameanza mchakato wa kukagua stakabadhi za wote waliotuma maombi, kabla ya kuchapisha majina inavyohitajika kisheria.
Shughuli ya kutuma maombi kwa kazi hiyo ilifungwa Jumamosi, Februari 15, saa kumi na moja jioni.
Baada ya kuwatathmini wote waliotuma maombi, jopo hilo litawasilisha majina ya watakaofaulu kwa Rais William Ruto kwa uteuzi.