Mshikilizi wa rekodi ya dunia Agnes Jebet, kushiriki Sirikwa Classic

Kulingana na Mkurugenzi wa mbio hizo, Barnaba Korir, ni wanariadha bora pekee kwenye msimamo wa dunia watakaoalikwa kushiriki.

Dismas Otuke
1 Min Read

Mshikilizi wa rekodi ya dunia katika mbio za kilomita kumi, Agnes Jebet Ngetich, ni miongoni mwa wanariadha waliotoa ithibati kushiriki makala ya nne ya mbio za nyika za Absa Sirikwa Classic, zitakazoandaliwa tarehe 22 mwezi huu eneo la Lobo Village, Kapseret mjini Eldoret.

Kulingana na Mkurugenzi wa mbio hizo, Barnaba Korir, ni wanariadha bora pekee kwenye msimamo wa dunia watakaoalikwa kushiriki.

Jebet atakayekuwa akishiriki mbio hizo kwa mara ya kwanza amesema atatumia kujiandaa kwa msimu huu ambao pia analenga kushiriki mbio za mita 5,000 na 10,000 kwenye mashindano ya dunia.

Wanariadha watashindana katika mbio za kilomita 2 kupokezana virojo, kilomita 10 wanaume na wanawake na chipukizi wasiozidi umri wa miaka 20.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *