Wizara ya fedha imepatwa na pigo katika juhudi za kutaka serikali ya kitaifa na zile za kaunti kugawana nakisi ya mgao wa bajeti.
Kamati ya kuwiainisha mabunge ya Seneti na la kitaifa, ilikataa pendekezo la kutaka nakisi hiyo ya pesa za matumizi kuachiwa serikali za ugatuzi.
Mbunge wa Kiharu Ndindi Nyoro aliyeongoza kamati hiyo, alisema mzigo wa nakisi ya pato kamwe haupaswi kuachiwa serikali za kaunti.
Haya yanafuatia hatua ya wizara ya fedha kuagiza bunge kukata shilingi bilioni 20 kutoka kwa bajeti ya shilingi bilioni 400, iliyotengewa serikali za kaunti kufuatia kufuatia kufutiliwa mbali kwa muswada wa fedha wa mwaka 2024.