Darassa achapisha orodha ya nyimbo za albamu yake mpya

Albamu hiyo kwa jina 'Take Away the Pain' ina jumla ya nyimbo 15 na amehusisha wasanii kadhaa maarufu wa ndani na nje ya Tanzania.

Marion Bosire
1 Min Read

Mwanamuziki wa mtindo wa rap nchini Tanzania Shariff Thabit Ramadhan maarufu kama Darassa amechapisha orodha ya nyimbo ambazo ziko kwenye albamu yake mpya.

Albamu hiyo kwa jina ‘Take Away the Pain’ ina jumla ya nyimbo 15 na amehusisha wasanii kadhaa maarufu wa ndani na nje ya Tanzania.

Wanamuziki waliohusishwa ni pamoja na Ali Kiba, Harmonize, Mbosso, Jay Melody, Kondela, Bien Aime, Zack Brown, Zuchu na Jovial.

Darassa anazindua albamu hii miaka minne tangu alipozindua albamu yake ya awali iitwayo ‘Slave Become a King’ ambayo ilifanya vizuri sana ndani na nje ya Tanzania.

“Hii ni tiba mbadala ya kiburudani. Hii ni albamu ya karne.” ndiyo maneno ambayo Darassa aliandika baada ya kutoa orodha ya nyimbo za albamu hiyo.

Alitoa shukrani kwa wote ambao walishirikiana naye akisema, “kwa pamoja tumetengeza hichi kitu bora sana kwa watu wetu. Mmetupa nguvu, moyo, muda pamoja na ujuzi wenu tunafahamu ni kitu cha thamani sana kwa mtu kutoa”.

Tazama orodha ya nyimbo hizo hapa;

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *