Mashabiki zaidi wataruhusiwa kuhudhuria mashindano ya mbio za magari ya WRC Safari Rally.
Kulingana na Afisa Mkuu Mtendaji wa WRC Safari Rally, Charles Gacheru, idadi kubwa ya mashabiki itaruhusiwa kwa mashindano ya mwaka huu kuliko makala yaliyopita.
Gacheru amefichua mashabiki watapewa uhuru wa kutangamana na madereva mashuhuri wa magari wakati wa mashindano.
Mabadiliko mengine katika mashindano ya mwaka huu ni kituo cha kuanzia ambacho kimehamishwa kutoka ukumbi wa KICC hadi nje ya City Hall.
Mashindano ya Kenya yataandaliwa kati ya Machi 20 na 23 yakiwa mkondo wa tatu wa msururu wa mashindano ya mwaka huu baada ya Monte Carlo, yaliyoandaliwa kati ya Januari 23 na 26 na Rally Sweeden yatakayoandaliwa baina ya Februari 13 na 16.