Mvua kuendelea kunyesha katika sehemu kadhaa za nchi

Tom Mathinji
1 Min Read
Mvua kuendelea kunyesha katika sehemu mbali mbali za nchi.

Mvua inayoshuhudiwa kwa sasa nchini inatarajiwa kuendelea kunyesha katika sehemu kadhaa juma hili.

Kulingana na Idara ya Utabiri wa Hali ya Hewa, mvua kubwa itashuhudiwa katika nyanda za juu eneo la kati mwa nchi, magharibi, Ziwa Victoria na nyanda za chini kusini mashariki mwa nchi hadi Jumamosi, Februari 1, 2025.

Hata hivyo, idara hiyo imedokeza kuwa sehemu nyingi katika eneo la Pwani, Kaskazini Mashariki na Kaskazini Magharibi mwa nchi zitashuhudia vipindi vya jua na anga kavu, huku maeneo kadhaa yakishuhudia mvua.

Kwa sasa, maeneo mengi jijini Nairobi yanashuhudia mvua kubwa inayosababisha mafuriko.

Mvua inatarajiwa kunyesha wakati wa asubuhi jijini Nairobi leo Jumatano na kisha kupisha vipindi vya jua.

Rasharasha za mvua zikiandamana na ngurumo za radi zitashuhudiwa sehemu kadhaa katika majira ya alasiri huku viwango vya joto vya juu vikiwa nyuzi 23 na vya chini nyuzi 17.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *