Awamu ya mwaka huu ya DKFF kuandaliwa Disemba

radiotaifa
1 Min Read

Awamu ya mwaka huu ya tamasha la filamu la watu walio na ulemavu wa kusikia yaani Deaf Kenya Film Festival – DKFF, itaandaliwa Disemba 2 na 3, 2024 katika taasisi ya Alliance Francais jijini Nairobi.

Tamasha hilo la kila mwaka liliasisiwa mwaka 2021 kwa lengo la kuwapa wabunifu wenye ulemavu ya kusikia fursa ya kukutana, kushirikiana na kuonyesha kazi zao.

Muungano wa wasanii wa Kenya wenye ulemavu wa kusikia “Deaf Artist Culture Association of Kenya – DACAK” ndio ulianzisha tamasha hilo.

Malengo mengine ya hafla hiyo ni kutoa uongozi, mafundisho na kutambua kazi zao kwa njia ya tuzo kando na kukutanisha wabunifu hao spesheli na wengine.

Vitengo vya tuzo hizo ni pamoja na filamu bora ya Kenya, mwandishi bora wa simulizi, mwigizaji bora wa kiume, mwigizaji bora wa kike, mwelekezi bora na mwigizaji msaidizi bora wa kiume na wa kike.

Share This Article