Bado nitasukuma kuondolewa kwa sheria ya fedha ya mwaka 2023 asema Omtata

Dismas Otuke
1 Min Read

Seneta wa Busia Okiya Omtata amesimama kidete kupinga sheria mpya ya fedha ya mwaka 2023 hadi ifutiliwe mbali na mahakama.

Akizungumza mahakamani Ijumaa punde baada ya mahakama ya rufani kuruhusu utekelezwaji wa sheria hiyo,Omtata alielezea matumaini ya kushinda kesi hiyo aliyowasilisha.

Mahakama ya rufani siku ya Ijuamaa, iliondoa marufuku iliyokuwa imewekwa na mahakama kuu, dhidi ya kutelezwa sheria hiyo.

Sheria hiyo inayopendekeza matozo mbalimbali kwa umma itatekelezwa ikusubiri uamuzi wa mwisho wa kesi yake Omtata.

Omtata na wakereketwa kadhaa waliwasilisha kesi mahakamani punde baada ya kuidhinishwa kwa sheria hiyo na Rais William Ruto kufuatia makabiliano makali wakati wa kupitishwa bungeni.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *