Mimba za mapema: Wanafunzi wa kike Kilifi wapewa ushauri nasaha

Glory Mwagambo
1 Min Read

Wadau mbalimbali katika kaunti ya Kilifi wamejitwika jukumu la kuwaleta pamoja wanafunzi wa kike waliobalehe kwa lengo la kuwapa nasaha hasa baada ya visa vya mimba za mapema kupungua katika kaunti hiyo.

Hatua hiyo inakuja wakati shule zikitarajiwa kufungwa wiki hii kwa likizo ndefu kote nchini.

Kupungua kwa visa vya mimba za mapema kunatokana na juhudi kabambe za wadau mbalimbali ambao wameeneza hamasa katika kaunti hiyo kuhusu umuhimu wa masomo na jinsi changamoto za wasichana shuleni zitakavyokabiliwa.

Akizungumza baada ya kukutana na zaidi ya wasichana 500 kutoka maeneo mbalimbali katika kaunti ya Kilifi, Afisa Mkuu wa Afya ya Uzazi Kennedy Miriti amesema kuwa visa vya mimba za mapema vimepungua kutoka asilimilia 33 hadi 12 kwa sasa.

Washika dau hao wanasema kuwa kuwajumuisha wanafunzi kwenye ushauri nasaha na jinsi ya kujikinga kumesaidia pakubwa kupungua kwa visa hvyo.

Nema Thuva ni mmoja wa wasichana aliyejifungua akiwa shuleni. Anasema kuwa amepitia changamoto si haba na kuwarai wanafunzi wenzake kutia bidii masomoni.

Glory Mwagambo
+ posts
Share This Article