Wananchi sisisi wamefurika katika Uwanja wa michezo wa Kwale huku sherehe za Mashujaa ziking’oa nanga.
Rais William Ruto ataliongoza taifa kuadhimisha sherehe hizo leo Jumapili katika kaunti hiyo ya Pwani Kusini.
Ruto alitua katika kaunti hiyo jana Jumamosi.
Malango ya Uwanja wa Kwale yalifunguliwa saa kumi alfajiri na kuwapa fursa wakazi wa Kwale kushuhudia sherehe hizo zikiandaliwa katika eneo hilo kwa mara ya kwanza.
Uwanja wa Kwale una uwezo wa kuwatoshea watu 10,000.