Kongamano la Magavana Wanawake kuandaliwa Kwale

KBC Digital
1 Min Read

Gavana Fatuma Achani anatarajiwa kuwa mwenyeji wa Magavana Wanawake 7 katika kaunti ya Kwale.

Achani atawaongoza Magava wenza katika uzinduzi wa kituo cha 2 cha saratani katika Ukanda wa Pwani kilichoko hospitali ya Kwale.

Kituo hicho kinalenga kupunguza dhiki ya wagonjwa wanaougua saratani hasa katika Ukanda wa Pwani.

Baadaye, Magavana hao watafululiza hadi studio za kurekodi muziki za kaunti hiyo na kisha waelekee katika uwanja wa Kwale kukagua ujenzi wa uwanja huo utakaotumika kwa sherehe za Mashujaa za mwaka huu.

Sherehe hizo zitakazoongozwa na Rais William Ruto zitafanyika siku ya Jumapili, Oktoba 20, ambayo ni Siku ya Mashujaa.

Wakati uo huo, Magava hao wakiongozwa na mwenyyeji wao Fatuma Achani watafululiza hadi hospitali ya Kinango ambapo watafungua mradi wa ujenzi wa kituo cha kusafisha figo na ujenzi wa chumba cha wagonjwa mahututi.

Aidha watazuru chuo cha walimu cha Kwale wanakotarajiwa kutoa hotuba wakiangazia masuala mbalimbali.

KBC Digital
+ posts
Share This Article