Waziri wa afya Dkt. Deborah Mlongo Baraza amewahimiza wakenya kuendelea kutembelea vituo vya afya, akihakikishia umma kwamba huduma za afya sasa zinatolewa chini ya halmashauri ya SHA, ambayo ilichukua mahala pa hazina ya kitaifa ya bima ya matibabu-NHIF.
Wakati wa ziara yake katika kaunti ya Mombasa siku ya Jumanne,Dkt. Barasa alitathmini ufanisi wa uzinduzi wa halmashauri ya SHA katika vituo kadhaa vya afya.
Barasa alipongeza ushirikiano kati ya serikali ya kaunti hiyo na halmashauri ya SHA, akitaja usaidizi kutoka kwa wafanyakazi wa kaunti ya Mombasa uliofanikisha mpito wa huduma za matibabu bila hitilafu,hususan katika upatikananji na utoaji wa matibabu muhimu kama vile uchunguzi wa kina wa saratani .
“Nahimiza vituo vyote vya afya kuendelea kuwahudumia wagonjwa bila wasiwasi,” alisema Dkt. Barasa akisema madeni yote yanayodaiwa na vituo hivyo vya afya yatalipwa na SHA.
Ziara hiyo yake ilijumuisha hospitali ya kihistoria ya Mombasa iliyoanzishwa miaka 130 iliyopita.
Vile vile waziri huyo alizuru hospitali ya rufaa na mafunzo ya Mombasa, kutathmini wa hudumza za SHA.