Gavana wa Kericho Erick Mutai leo Jumatano amejipata matatani baada ya wawakilishi wadi katika bunge la kaunti hiyo kupiga kura ya kuunga mkono hoja ya kumtimua madarakani.
Awali, Gavana Mutai alienda mahakamani kuzuia kutimuliwa kwake.
Hata hivyo licha ya agizo la mahakama la kuzuia kutimuliwa kwake, wawakilishi wadi 31 walipiga kura ya kuunga mkono hoja ya kutaka Gavana Mutai afurushwe madarakani.
Miongoni mwa masuala mengine, wanamtuhumu kwa kuwa na mienendo mibaya inayojumuisha unyanyasaji wa kingono na ukiukaji wa katiba.
Gavana Mutai sasa atalazimika kufika mbele ya bunge la Seneti kujitetea kuhusiana na tuhuma dhidi yake.
Anakuwa Gavana wa pili kukumbana na makali ya wawakilishi wadi katika siku za hivi karibuni baada ya Gavana wa Meru Kawira Mwangaza kupitia wembe huohuo.