Wafanyakazi kadhaa wa vyuo vikuu leo Jumatatu wamekamatwa na polisi wakiandamana jijini Nairobi wakidai nyongeza ya mshahara.
Polisi pia wamewarushia vitoza machozi waandamanajii hao kwa kukaidi amri ya kutofanya maandamano katikati ya jiji.
Wafanyakazi hao wanagoma kuishinikiza serikali kutekeleza nyongeza ya mshahara kwa mujibu wa mkataba wa maelewano (CBA) wa mwaka 2021-2025.
Shughuli za kawaida vyuoni zimekwama tangu wafanyakazi hao waanze mgomo wa kitaifa.