Kisa cha pili cha Mpox charipotiwa hapa nchini

Tom Mathinji
1 Min Read

Wizara ya afya imeripoti kisa cha pili cha ugonjwa wa Mpox humu nchini.

Waziri wa afya  Deborah Barasa, alisema mgonjwa huyo ni mwanamume mwenye umri wa makamo ambaye aligunduliwa katika kituo cha mpakani cha Malaba, kaunti ya Busia baada ya kuonyesha dalili za ugonjwa huo.

Alisema mgonjwa huo alikuwa akisafiri kutoka taifa la Jamuhuri ya kidemokrasia ya kongo ambako ni chamko la ugonjwa huo.

Daktari Barasa alisema mgonjwa huyo ametengwa na anazuliwa katika kituo cha afya katika kaunti ya Busia.

Kadhalika alisema, uchunguzi umeimarishwa wa visa vinyavyoshukiwa kuwa wa ugonjwa huo katika eneo hilo na katika kaunti zote ili kuhakikisha msambao wa ugonjwa huo unadhibitiwa.

Waziri alisema kufikia sasa jumla ya sampuli 42 zilizowasilishwa kwenye maabara kwa uchunguzi wa ugonjwa wa Mpox, sampuli 40 hazikuonesha maambukizi hayo. Aidha wizara ya afya imewachunguza jumla ya wasafiri elfu 426,438 kwenye vituo vya mipaka ya kuingia humu nchini.

Dkt. Deborah hata hivyo amesisitiza kuwa vituo vya afya vina vifaa vya kutosha kuchunguza na kudhiti ugonjwa huo.

Share This Article