Gwiji wa muziki Eric Wainaina amezindua wimbo wa nne mwaka huu wa 2024 unaofahamika kama “Ũke”.
Wimbo huo uliotolewa rasmi Ijumaa Agosti 16, 2024, unahimiza watu kuja pamoja. Unahimiza msikilizaji;
Kuleta mama na kumwonyesha kwamba anapendwa na,
Kuleta baba pia ili asijihisi mpweke.
Anahimizwa pia kuleta ndugu sio kuja kuwazaba makofi,
Lakini amlete shangazi,
Yeye ndiye anajua kucheza!
Wimbo huo unaangazia wanachama wa bendi ya Eric akiwemo mpiga ngoma Mbogua Mbugua Mbugua, Benja Kabaseke ‘Ladies!’ Masinde mcheza gitaa, Victor Kimetto na Eric wanaocheza kibodi naye Asaph Uzele anayecheza Bass gitaa.
Eric na Mbogua Mbugua Mbugua walihusika katika kupanga na kuandaa kibao hicho huku waimbaji Kendi Nkonge, Charity Nyambura, Sho, Tim Arinaitwe, Matt Ngesa na Vini Ngugi wakitia sauti zao.
Alex Mottok alihusika na mpangilio wa ala za muziki.
Wimbo “Ũke” unapatikana kwenye majukwaa yote ya kidijitali.